# Taarifa ya jumla Sila na Timotheo walioungana na Paulo # Kwahiyo Paulo akajadiliana Hapa "kujadiliana" inamaanisha Paulo alikuwa na maongezi ya pande mbili". "kwa hiyo walijadiliana" # Aliwashawishi "aliendelea kujaribu kuwashawishi" # Paulo alisukumwa na Roho Paulo alizidi kusukumwa na Roho. # akakung'uta vazi lake Hii ni hatua ya mfano zinaonyesha kwamba Paulo alikata mahusiano na Wayahudi wasioamini na kuwaacha kwa hukumu ya Mungu. # Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu wenyewe Hapa "damu" inalinganishwa na adhabu ya dhambi. Paulo anawaambia Wayahudi hao kuwa watawajibika kwa ajili ya hukumu watakayokabiliana nao kwa sababu ya ukaidi wa kukataa kutubu. "Ninyi peke yenu mtabeba jukumu la adhabu yenu kwa ajili ya dhambi zenu".