# Taarifa ya jumla Hii ni sehemu nyingine ya hadithi ya Paulo na Sila wakiwa safarini. Paulo kwa sasa yuko Athene akiwangojea Silas na Timotheo kuungana naye. # roho yake iikasirishwa kuona mji umejaa na miungu ya sanamu. "alisumbuliwa" au "alifadhaika" au "akawa na huzuni" # akajadiliana Hili neno linaashiria kuwa kulikuwa na majibizano zaidi kutoka kwa wasikilizaji kuliko katika kuhubiri. "alijadiliana" # sokoni Hii ni sehemu ambayo watu huuza na kununua vitu, ngombe, au huduma hutolewa. " sehemu ya umma" # Wale waliokuwa wakimwabudu Mungu Inamaanisha Watu wa mataifa waliokuwa wakimsifu Mungu na kumfuata ingawa hawakuwa wakifuata taratibu za ibada ya Kiyahudi.