# Kauli Unganishi: Paulo na Barnaba wanaendelea kuzungumza na kundi nje ya mji wa Listra. # hakujiacha mwenyewe bila ya shahidi Hii inaweza pia kuwekwa katika hali chanya. "hakika Mungu ameacha shuhuda" au "hakika Mungu ameshuhudia" # kwa kuwa "kama inavyooneshwa na ukweli kuwa" # akiwajaza mioyo yenu kwa chakula na furaha Hapa "mioyo yenu" inamaanisha watu. "akiwapa cha kutosha kula na vitu ambavyo vitawapa furaha" # Paulo na Barnaba wakawazuia makutano kuwatolea sadaka kwa nadra Paulo na Barnaba waliwazuia makutano kuwatolea sadaka, lakini ilikuwa ni taabu kufanya hivyo. # wakawazuia ... kwa nadra "walikuwa na wakati mgumu kuwazuia"