# Kauli Unganishi: Paulo na Barnaba sasa wako Listra. # Taarifa ya Jumla: Taarifa ya Jumla: Anayezungumziwa kuwa na imani ni yule kiwete; na aliyemsemesha ni Paulo. Yule aliyesemeshwa ni kiwete. # mtu fulani aliketi Hii inatambulisha mtu mpya katika simulizi. # dhaifu miguuni mwake "kutokuweza kusogeza miguu yake" au "kutokuweza kutembea kwa miguu yake" # kiwete "kilema" # kiwete tangu tumboni mwa mama yake "kiwete tangu kuzaliwa" # Paulo alimkazia macho "Paulo alimtazama moja kwa moja" # alikuwa na imani ya kufanywa mzima Nomino "imani" inaweza kutafsiriwa kama kitenzi "amini." "aliamini kwamba Yesu anaweza kumponya" au "aliamini kuwa Yesu anaweza kumfanya mzima" # akaruka juu "akaruka hewani." Hii inaashiria kwamba miguu yake ilikuwa imeponywa kikamilifu.