# Sentensi unganishi Paulo anaanza hotuba yake kwa watu waliokuwamo kwenye Sinagogi huko Antiokia ya Pisidia. Anaanza kwa kuzungumzia mambo ambayo yalitokea katika historia ya Israeli. # alisimama na kuwapungia mkono Inamaanisha kutoa ishara kwa mikono kwamba yuko tayari kuanza kusema. # enyi mnao mtii Mungu Anamaanisha, Wamataifa ambao wanafuata desturi na dini ya Kuyahudi. "Ninyi msio Waisrael, lakini mnamwabudu Mungu" # sikilizeni "Nisikieni mimi" au "Sikieni ambacha nataka kuwaambia" # Mungu wa hawa watu wa Israeli "Mungu ambye anaabudiwa na Waisraeli # baba zetu "Mababa wa Wayahudi" # na kuwafanya watu wengi "Aliwawezesha wao kuwa watu wengi sana" # kwa mkono wake kuinuliwa anamaanisha Mkono wa Mungu wenye uweza. # aliwaongoza nje yake "Kutoka katika nchi ya Misri" # aliwavumilia linamaanisha "Aliwajali" na "Aliwavumilia katika kutokutii kwao"