# Maelezo ya jumla Hapa Petro anajumuisha yeye, Mitume na Wayahudi waumini wote waliopokea Roho Mtakatifu katika siku ya Pentekoste. # Nilipoanza kusema nao, Roho mtakatifu akaja juu yao namaanisha kwamba, "Petro kabla hajamaliza kunena, kwa vile alikuwa amenuia kusema nao zaidi, Roho Mtakatifu akaingilia kati kwa kuwashukia. # Roho mtakatifu akaja juu yao kama alivyokuja kwetu mwanzoni. Roho Mtakatifu alishuka kwa wamataifa walioamini kama vile alivyofanya kwetu siku ya Pentekoste. # mtabatizwa katika Roho mtakatifu Mungu atawabatizeni ninyi katika Roho Mtakatifu.