# Sentensi unganishi Petro anaanza hotuba kuongea na kila mtu ndani ya nyumba ya Kornelio. # Ndipo Petro akafungua mdomo wake na kusema "Petro alianza kuzungumza kwao" # Hakika Hii inamaanisha kile anachokwenda kukisema kina umuhimu wa kukijua # Mungu hawezi kuwa na upendeleo "Mungu hapendelei watu maalumu" # kila mtu yeyote anayemwabudu na kufanya matendo ya haki anakubalika kwake "anamkubali kila mtu anayemwabudu na kufanya matendo ya haki" # Ibada Neno "Ibada" linamaanisha nia ya ndani ya heshima na kicho cha kweli.