# akiwaza juu ya hayo maono "Wakati Petro alipokuwa akifikri juu ya haya maono" # Roho "Roho Mtakatifu" # Tazama Uwe macho" au "Amka" # watu watatu wanakutafuta Baadhi ya nyaraka za kale zinasema idadi tofauti ya wale watu. # Shuka chini "Shuka chini kutoka dari ya nyumba" # Usiogope kwenda nao Ingekuwa kawaida kwa Petro kutokwena na hao watu; 1) Kwa vile walikuwa wageni kwake na 2) Walikuwa wa mataifa ambapo Wayahudi walikuwa hawachangamani na wao. # Mimi ni yule mnayemtafuta "Mimi ndiye mtu yule mnayemtafuta"