# Sentensi unganishi Simlizi ya Tabitha inaishia katika mstari 42, na mstari 43 unatuambia kilichokuwa kinaendelea kwa Petro baada ya simlizi ya Tabitha kumalizika. # Akawatoa wote nje Kwa shauri hili, Petro aliwafanya kila mmoja kuondoka ili aweze kuwa pekee yake na kuomba kwa ajili ya Thabitha. # akampa mkono wake akamwinua Petro alimshika mkono wake na kumsaidia kuinuka. # waumini na wajane, Hata wajane yawezekana walikuwa waumini, lakini hapa wametambulishwa kwa jina la wajane kwasababu Tabitha alikuwa mtu muhimu kwao. # Jambo hili kujulikana Yafa yote Muujiza wa Petro kumfufua Tabitha kutoka kwenye kifo ukajulikana na watu wote wa Yafa. # Walimwamini Bwana "waliiamini injili ya Bwana Yesu." # Ikatokea kwamba Petro alikaa "Ikatokea kuhusu kwamba Petro akakaa huko kwa muda"