# Wayahudi Inamaanisha Wayahudi viongozi. # lakini mpango wao ukajulikana na Sauli "Lakini mtu mmoja akawaambia mpango wao kwa Sauli" au "Lakini Sauli akafahamu mipango yao juu yake" # Wakamvizia mlangoni Mji huu ulikuwa na ukuta uliouzunguka.Watu waliingia na kutoka katika mji huo kupitia mlango. # Wanafunzi wake Watu walioamini ujumbe wa Sauli kuhusu Yesu na walifuatilia mafundisho yake # wakamshusha kupitia ukutani, wakamtelemsha chini katika kapu Kwa kutumia kamba walimshusha Sauli katika kikapu kikubwa kupitia tundu katika ukuta.