# Maelezo ya jumla Hiki ni kifungu kutoka katika kitabu cha Isaya # Kama kondoo mbele ya mchungaji akiwa kimya Mkata manyoya ni mtu ambaye anakata manyoya ya sufu za kondoo ili zitumike. # Kwa kuhuzunishwa kwake hukumu yake iliondolewa Alidharauliwa na kuhukumiwa bila haki. # Nani ataeleza kizazi chake? Swali hili lilitumika kuelezea kuwa hatakuwa na uzao. Kwamba; "Hakuna hata mmoja atakayeweza kuzungumzia habari za uzao wake" # maisha yake yameondolewa katika nchi." Hii inaelezea kifo chake. "Watu walimwua" au "Watu waliyaondoa maisha yake hapa duniani"