# Sentensi unganishi Luka anaendeleza habari ya kile kilichokuwa kinatokea huko Samaria. # Wakati mitume wa Yerusalemu waliposikia Alama hii ni ya mwanzo wa sehemu mpya ya simlizi ya waumini walivyokuwa wakiendelea huko Samaria. # Samaria "Samaria" Neno linaloelezea juu ya watu wengi waliokuwa waumini katika wilaya yote ya Samaria. # Pale waliposhuka chini "Pale Petro na Yohana waliposhuka chini" kwenda Samaria. # Waliomba kwa ajili yao "Petro na Yohana waliwaombea waamini wa Samaria" # Kwamba wangepokea Roho Mtakatifu. "Kwamba Wasamaria wanaoamini wangeweza kupokea Roho Mtakatifu" # Walikuwa tu wamebatizwa "Filipo alikuwa tu amewabatiza katika Jina la Bwana Yesu Wasamria walioamini" # Ndipo Petro na Yohana wakaweka mikono yao kwao "Kwao" linahusu watu wa Wasamaria ambao waliamini ujumbe wa injili kutoka kwa Filipo".