# Sentensi unganishi Sehemu ya habari kuhusu Stefano iliyoanzia sura 6:8 inaendelea. Stefano anaanza kumjibu Kuhani Mkuu na baraza kwa kuanza kuzungumzia mambo yaliyotukia katika historia ya Israeli. Maelezo mengi ya Stefano yanatoka kwenye vitabu vya sheria vya Musa. # Maelezo ya ujumla Kwenye mstari wa 2,Stefano anaanza hotuba yake kumjibu kuhani mkuu na baraza.Anaanza hotuba yake kwa kuongelea mambo yaliyotokea katika historia ya Israeli. # Ndugu na baba zangu,nisikilizeni mimi. Stefano alikuwa akiheshimika sana kwenye baraza kwa salamu yake ya kifamilia.