# Wanaume wa Israeli, iweni makini sana na kile mnachopendekeza kuwafanyia watu hawa Gamarieli anawaeleza majumbe wa baraza wasifanye jambo lolote juu ya hao mitume litakalowaletea majuto baadaye # Theuda aliinuka na kujidai kuwa mtu mkuu Theuda alikuwa ameasi na kujitwalia idadi kubwa ya wafuasi # Aliuawa, na wote waliokuwa wanamtii walitawanyika Watu walimwua na jamii ikatawanyika. # Baada ya mtu huyu, Yuda mgalilaya, aliinuka siku zile za kuandikwa sensa, akavuta watu wengi nyuma yake. Yuda Mgalilaya naye vilevile alitokea wakati wa sensa ya Kaisari, aliwavuta wengi kuasi dhidi ya utawala wa dola ya Kirumi kisha naye kapotea.