# Petro na mitume wakajibu Petro alizungumza kwa niaba ya mitume wote kwa maneno yafuatayo. # kwa kumtundika juu ya mti Petro anatumia neno "mti" kuonyesha kuwa msalaba ulitengenezwa kutokana na mti. "Kwa kumtundika juu ya msalaba" # kutoa toba kwa Israeli, na msamaha wa dhambi Neno "toba" na "msamaha" yanamaanisha kuleta msamaha kwa watu wa Israeli kwa njia ya toba na kisha Mungu kuwasamehe dhambi zao. # Israeli Linamaanisha Wayahudi wote. # kwa wale wanaomtii "Wote wanaojikabidhi chini ya mamlaka ya Mungu"