# Sentensi unganishi Mlinzi na maafisa waliwaleta mitume mbele ya baraza la viongozi wa dini. # waliwaogopa watu Mitume walipelekwa bila vurugu mbele ya baraza, viongozi walikuwa wamewahofia watu juu ya kitendo chochote wangekifanya kwa mitume. # Katika jina hili Neno "Jina" linamaanisha Yesu Kristo. Mitume walizuiliwa wasinene neno lolote kupitia Jina la Yesu. # mmeijaza Yerusalemu kwa fundisho lenu Inamaanisha wamewafundisha watu wote wa Yerusalemu habari za Yesu. # na kutamani kuleta damu ya mtu huyu juu yetu. Neno "Damu" linamaanisa kifo cha Yesu na damu yake. Kwamba Viongozi hao walipaswa kuwajibika kwa kuhusika kwao kumwua Yesu Kristo.