# Nendeni, mkasimame hekaluni Mitume walikwenda kusimama hekaluni katika ile sehemu ya wazi, hawakuingia ndani ambamo hawaruhusiwi kuingia ispokuwa kwa makuhani tu. # maneno yote ya Uzima huu. Hii inamaanisha ujumbe wa Injili ambao mitume walikuwa wakiutangaza. # wakati wa kupambazuka Ilipoanza kuwa nuru, "Ingawa malaika alikuwa amewatoa mitume jela wakati wa usiku, hivyo kulipoanza kupambazuka mitume walikuwa tayari wamefika hekaluni. # kuwatuma gerezani ili kuwaleta mitume. Inamaanisha kuhani alituma mmoja wao kwenda gerezani kuwachukua mitume na kuwaleta mbele ya baraza.