# Kisha, Petro, akiwa amejaa Roho Mtakatifu Roho Mtakatifu akiwa amemjaza Petro. # kama sisi siku ya leo tunahojiwa kuhusu tendo jema lililofanywa kwa mtu huyu mgonjwa - kwa namna gani mtu huyu alifanywa mzima? Petro aliuliza swali hili kufafanua kwamba ilikuwa sababu halisi ya kuteswa kwao. Mnatuuliza leo kwa namna gani mtu huyu amepata kupona. # Hebu lijulikane hilo kwenu na kwa watu wote katika Israel Na ijulikane kwenu na watu wote wa Israel kujua hili. # kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, Neno "Jina" linafafanua nguvu na mamlaka ya jina hilo. Kwa mamlaka ya Jina la Yesu Kristo wa Nazarethi.