# Sentensi unganishi Huu ni mwisho wa sehemu ya habari kwa tukio la siku ya Pentekoste. Inaanza sehemu nyingine inayoelezea jinsi gani waumini waliendelea kuishi baada ya siku ya Pentekoste. # alishuhudia na kuwasihi "Aliwaambia waziwazi na kuwasihi waitikie kwa ujumbe alioutoa kwao. # Jiokoeni mtoke katika kizazi hiki kiovu Wajiokoe kutoka katika adhabu ya Mungu itakayowapata watu waovu. # wakayapokea maneno yake Inamaanisha wakayapokea maneno aliyoyasema Petro kuwa yalikuwa ya kweli. # Walibatizwa Wote walioamini walibatizwa. # hapo wakaongezeka katika siku hiyo kama watu elfu tatu "watu wapatao elfu tatu waliongezeka" # katika kuumega mkate Walishiriki na kula chakula kwa pamoja