# Maelezo ya jumla Petro ananukuu kifungu ambacho Daudi alikiandika katika Zaburi kinachotaja kuteswa kwa Yesu na kufufuka kwake. # Maelezo ya jumla Tangu Petro ataje kwamba Daudi alitangulia kusema maneno kuhusu Yesu, maneno "Mimi na Yangu" yanamtambulisha Yesu. Na maneno Bwana na Yeye" yanamtambulisha Mungu. # mbele ya uso wangu Linamaanisha, "Mbele yangu au mbele ya uwepo wangu" # pembeni mkono wangu wa kulia Mkono wa kulia ulifikiriwa kuwa ni wa nguvu sana. Mtu aliye mkono wa kuume alikuwa ama mtumishi mwenye nguvu sana au msaidizi mwenye uwezo sana. # moyo wangu ulikuwa na furaha na ulimi wangu ulishangilia. NI: "Nilikwa na furaha na kushangilia" # mwili wangu utaishi katika ujasiri "Ingawa hata mimi ni wa kufa tu, nitakuwa na ujasiri kwa Mungu"