# Maelezo ya jumla Mstari wa 5 unatoa taarifa ya nyuma kuhusu idadi kubwa ya wayahudi ambao walikuwa wanaishi Yerusalemu, wengi wao walikuwapo wakati wa tukio hili. # Maelezo ya jumla Hapa neno "wao" linajumuisha waumini na neno "yake" linataja kila mtu katika kundi. # watu wa Mungu watu waliotaka kuheshimu na au kumwabudu Mungu # kila taifa chini ya mbingu "kila taifa duniani" Watu kutoka mataifa mbalimbali walikuwa wamekuja Yerusalemu. # Wakati sauti hii iliposikika Hii inarejea sauti ambayo ilikuwa kama upepo wa nguvu kuwa: "Waliposikia sauti hii" # Mkusanyiko "kundi kubwa la watu" # Walishangaa kwa mshangao mkuu Maneno haya yana maana moha. Mshangao wao ulikuwa mkuu sana. # Kweli, hawa wote wanaoongea siyo Wagalilaya? Watu waliuliza swali wakionyesha mshangao wao kuwa hawa ni wa eneo moja na lugha yao ni moja iweje waongee na lugha za mataifa yetu?