# Sentensi unganishi Yohana anatuma salaam kwa Gayo # Maelezo ya jumla Hii ni barua mtu binafsi Yohana anaituma kwa Gayo. Maneno yote ya kiwakilishi cha majina yanamtaja Gayo katika umoja. # Mzee Ni kiwakilishi cha Yohana, mtume na mwanafunzi wa Yesu. Yeye mwenyewe anajiwakilisha kama "mzee" pengine kwa sababu ya umri wake au kwasababu ya uongozi wake wa kanisa. Jina la mwandishi linaweza kufupishwa: Mimi, Yohana mzee, ninaye andika. # Gayo Huyu ni mshirika mwamini ambaye Yohana anamwandikia barua hii. # Ambaye ninayempenda katika kweli "Ambaye ninampenda kweli" # Unaweza kufanikiwa katika mambo yote na kuwa na afya "Unaweza kufanya mambo yote vizuri na kuwa na afya" # Kama na roho yako ifanikiwavyo "Kama vile unavyoendelea vizuri kiroho" # Ndugu "washirika waumini" # dhihirisha ushuhuda wa kweli yako, kuwa unatembea katika kweli "aniambia kuwa unaishi kulingana na ukweli wa Mungu" # Wanangu Yohana anazungumzia wale aliowafundisha kumwamini Yesu kama vile watoto wake. Hii inauelezea upendo wake na nia yake kwa ajili yao. Inaweza pia kuwa yeye mwenyewe aliwaongoza kumjua Bwana. "Watoto wangu wa kiroho"