# Kimbieni tamaa za ujana Mafumbo haya yanamaanisha mbio haraka uwezavyo. Kukimbia ni kukimbia kitu kitakachoweza kuwadhuru ninyi, kufuata ni kukimbia kuelekea kitu ambacho kitakufanyia mema. # ukafuate haki "kuitafuta haki" # Na Maana inawezekana ni 1) Paulo alimtaka Timotheo kujiunga na wakristo wengine katika kutafuta haki' au 2) Paulo alimtaka Timotheo awe na amani na sio kugombana na waamini wengine. # nao wamwitao Bwana "Wakristo" au "wote ambao wanaojiita watu wa Mungu" # kwa moyo safi "Kwa nia ya dhati" au "kwa sababu nzuri" # ukatae upumbavu na maswali ya kipuuzi "Kukataa kujibu maswali ya upumbavu" na "maswali ya kipuuzi" # Moyo safi Paulo anazungumza juu ya sababu nzuri za kufanya jambo toka moyoni. # Huzaa ugonvi Paulo anazungumza juu ya maswali ya kipuuzi akiyafananisha na mwanamke anayezaa mtoto. "inasababisha ugonvi"