# Maelezo ya Jumla: Paulo anawapa waumini maelekezo ya mwisho kuhusu kufanya kazi na sio kukaa bila kufanya kazi. # Sasa Paulo anatumia neno hili kuonyesha kubadili mada. # katika jina la Bwana Yesu Kristo "kwa mamlaka ya Yesu" # ndugu hapa "ndugu" linamaanisha wakristo wenzetu, inajumuisha wote wanaume na wanawake. AT: "ndugu wa kiume na wakike" # Bwana wetu Neno "wetu" linamaanisha waumini wote. # kuishi bila kufanya kazi "ni mzembe na anazuia kufanya kazi" # kutuiga sisi " kufanya kama Paulona wenzake" au " kutenda kama Paulo na watenda kazi wenzake' # Hatukuishi kati yenu kama wale wasio na nidhamu Paulo anatumia maneno hasi ili kusisitiza maneno chanya. AT: "Tuiishi miongoni mwenu kama waliokuwa na nidhamu sana" # tulifanya kazi usiku na mchana "tulifanya kazi wakati wa usiku na wakati wa mchana" au "tulifanya kazi muda wote" # katika kazi ngumu na shida Paulo anasisitizajinsi hali yake ilivyokuwa ngumu. kazi ngumu inamaanisha kazi ambayo inahitaji juhudi kubwa. Ugumu inamaanisha walivumia maumivuna mateso.AT: "katika hali ngumu. # Tulifanya hivi sio kwa sababu hatukuwa ma mamlaka Paulo anatumia neno hasi kusisitiza upande chanya. Hii inaweza kusemwa kama chanya. AT: "pasina shaka tulikuwa na mamlaka."