# Maelezo ya Jumla: Paulo anawaomba waumini waombe kwa ajili yake na wenzake # Na sasa Paulo anatumia neno "sasa" kubadilisha mada. # ndugu hapa neno "ndugu" linamaanisha wakristo wenzetu, linajumisha wanaume na wanawake. AT: "ndugu wa kiume na wakike" # neno la Bwana liweze kuenea na kutukuzwa Paulo anaongea kutawanya kana kwamba Neno la Mungu linakimbia toka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. AT: "kwamba watu wengi zaidi na zaidi hivi karibuni watasikia ujumbe wetu kuhusu Bwana wetu Yesu na kuuheshimu" # kwamba tuweze kuokolea Hili linaweza kusemwa katika muundo tendaji: AT: "kwamba Mungu atuokoe" au " kwamba Mungu aweze kutuokoa sisi" # Kwa sababu sio wote wanayo imani "kwa kuwa watu wengi hawaamini katika Yesu" # ambaye atawaimarisha ninhyi "ambaye atawaimarisha ninyi" # yule mwovu "Shetani"