# Maelezo ya Jumla: Paulo ndiye mwandishi wa barua hii, lakini anawajumuisha Silwano na Timotheo kama wapelekwaji wa barua. Anaanza kwa kusalimia kanisa la Thesalonike. # Maelezo ya Jumla: Maneno "sisi" linamaanisha Paulo, Silwano naTimotheo, au kama limetumika vinginevyo. Pia neno " ninyi" ni wingi na lina maanisha waumini wa kanisa la Wathesalonike. # Silwano Huu ni muundo wa Kilatini "Silas." Ni mtu yule yule aliyeorodheshwa katika kitabu cha Matendo kama msafiri mwenzi wa Paulo. # Neema iwe juu yenu Paulo kawaida anatumia salamu hii katika barua zake.