# Maelezo ya Jumla: Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea # hii ngao ya wokovu wako Daudi anailinganisha nguvu ya Yahwe ya kuokoa sawa na ngao inayomkinga askari na adui yake. # Matakwa yako Mungu alijibu maombi ya Daudi na kumpa baraka na mafanikio juu ya adui zake # 7Umeitengenezea miguu yangu nafasi chini yangu Yahwe amemweka Daudi mahala salama ambapo adui zake hawawezi kumnasa. "Miguu" inamaanisha uwezo wa Daudi wa kusimama salama.