# Maelezo ya Jumla: Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea. # Maana ni nani aliye Mungu isipokuwa Yahwe? Na ni nani aliyemwamba isipokuwa Mungu? Daudi anatumia maswali kusisitiza kwamba hakuna Mungu zaidi ya Yahwe. # aliyemwamba Daudi anamlinganisha Yahwe na mwamba kusisitiza nguvu zake na uwezo wa kuwalinda watu wake. # humwongoza asiye na hatia katika njia yake Yahwe humlinda asiye na hatia katika usalama na kuondoa kila kinachoweza kumdhuru.