# Maelezo ya Jumla: Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea. Anatumia usambaba kusisitiza akisemacho # Alizifungua mbingu... akamwaga mawingu angani Daudi anazungumzia njia za Yahwe kwa kumwokoa Daudi kutoka kwa adui zake kama mawingu ya dhoruba yakusanyikayo juu ya sehemu. Hii inasisitiza nguvu za Mungu na hasira yake. # chini ya miguu yake Daudi anamzungumzia Mungu kama ana miguu ya watu. # Alionekana katika mawingu ya upepo Yaweza kuwa "alionekana juu ya mawingu ya upepo" # mawingu ya upepo Hii inaonesha upepo kama ulikuwa ni ndege # Na akafanya giza hema kumzunguka Giza alilolifanya Yahwe linalinganishwa na hema limfichalo kabisa.