# Maelezo ya Jumla: Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea. Anatumia usambaba kusisitiza akisemacho # Kisha nchi ilitikisika... ikawashwa kwayo Hili ni jibu la Yahwe kwa kilio cha Daudi msaada kutoka kwa adui zake. Daudi anatumia taswira ya dunia kutikisika na moto kutoka kwa Yahwe kusisitiza hasira kari ya Yahwe. # Dunia ilitikisika... mbingu zikatetemeka Daudi anazungumzia mitizamo hii miwili kuhusisha kila kitu katika uumbaji. # na ilitikiswa , kwa sababu Mungu alikuwa na hasira. Hii yaweza kumaanisha "kwa sababu hasira ya Mungu ilizitikisa." # mianzi ya pua yake... kinywa chake Daudi anamzungumzia Yahwe kama vile alikuwa na sehemu hizi za wanadamu. # Makaa yaliwasha kwayo Hapa hasira ya Yahwe inalinganishwa na moto, uliosababisha makaa kuwashwa.