# Maelezo ya Jumla: Wimbo wa Daudi kwa Yahwe unaendelea. Anatumia usambaba kusisitiza akisemacho # Katika shida yangu "katika taabu zangu kubwa" # akaisikia sauti yangu katika hekalu lake, Daudi anamaanisha hekalu la mbinguni anapoishi Yahwe. Hekalu la duniani lilikuwa bado kujengwa. # kilio changu cha msaada kikafika masikioni mwake Usemi wa "masikio yake" inaonesha Yahwe akisikiliza kilio cha Daudi kwa msaada.