# Naapa kwa Yahwe Yoabu anafanya nadhiri madhubuti. # Usipokwenda, hakuna mtu hata mmoja atakayebaki Hii inamaanisha kwamba askari wangebaki iwapo tu Daudi angekwenda. # Hakuna atakayesalia Hii inaonesha wao kubaki watiifu kwake. # Wote wakaambiwa Hii inaweza kuelezwa kuwa wengi wao. # Tazama Hii imetumika kuvuta makini ya mtu kwa ajili ya habari inayofuata. # Watu wote Hapa "watu" inahusu waliomfuata Daudi. # Israeli walikimbia kila mtu nyumbani kwake Hapa "Israeli" inahusu askari wa Waisraeli waliomfuata Absalomu.