# Ikatukia kwamba Absalomu akakutana na askari wa Daudi Hili ni tukio lilotokea wakati wa vita. # na kichwa chake kikanaswa katika matawi ya mti Absalomu alikuwa na nywele ndefu zilizonasa kwenye matawi ya mti. # Tazama Neno hili linavuta makini ya mtu kwa ajili ya kinachofuata. # Ning'inia Kuelea juu bila kukanyaga juu ya nchi au kitu. # kati ya nchi na anga "Hewani" # Kwa nini haukumpiga hata chini Swali hili linamaanisha alipaswa kuwa amemuua. # shekeli kumi za fedha na mkanda Katika viwango vya sasa ni sawa na gramu 110 za fedha. # mkanda Huu ni mkanda maalumu unaoonesha kwamba mtu fulani ni askari mwenye cheo ili apewe heshima.