# Ahithofeli Hili ni jina la mwanamme # kulitunza kasiri Kifungu "kutunza" kinamaanisha kuangalia. # kuwa kitu kinachonuka mbele ya baba yako Ahithofeli anazungumia Absalomu kumchukiza baba yake kama vile kingekuwa kitu ambacho kina harufu ya kuchukiza. # Kisha mikono ya wote walio pamoja nawe itatiwa nguvu Hapa watu waliomfuata Absalomu wanarejerea kwa kutaja mikono yao. Habari hii itaitia nguvu utiifu wa watu kwa Absalomu na kuwapa hamasa.