# Je haunao pamoja nawe Sadoki na Abiathari makuhani? Daudi anauliza swali hili ili kumwambia Hushai kwamba hayupo peke yake. Yaani kuonesha kwamba "Sadoki na Abiathari makuhani watakuwepo kukusaidia." # chochote unachosikia... lolote usikialo Hii ni kuzidisha maana; haimaanishi kila neno asikialo. Inamaanisha mambo muhimu ayasikiayo. # Ahimaasi... Yonathani Haya ni majina ya watu. # Kwa mikono yao Kifungu "mikono yao" kinarejerea kwa wana na kinamaanisha kwamba wangehudumu kama wajumbe.