# Mioyo ya watu wa Israeli inaambatana Hapa watu wanarejerewa kwa "mioyo" kusisitiza utiifu wao kwa Absalomu. # kujiepusha na Absalomu... kwa haraka... na ataleta Hapa Daudi anaongelea Absalomu na watu aliokuwa nao kama "Absalomu" yeye mwenyewe kwa sababu watu walikuwa wanafuata mamlaka ya Absalomu. # kuushambulia mji kwa ukali wa upanga "Mji" unatajwa kuonesha watu wa mji. "Ncha ya upanga" inarejerea kwa panga za waisraeli kusisitiza kwamba waliwaua watu vitani. # kusababisha madhara Hii inamaanisha kusababisha madhara kutokea.