# Basi "Basi" inaonesha badiliko katika habari kuu. Hapa Samweli anatoa sehemu nyingine ya habari. # Hakukuwa na mtu katika Israeli aliyesifiwa kwa uzuri kama Absalomu Watu walimsifu Absalomu kwa uzuri wake wa sura kuliko walivyomsifu mwingine yeyote. # Kutoka katika wayo wa mguu wake hadi katika utosi wake hakuwa na waa lolote Hii inamaanisha kwamba hakuwa na kasoro. # shekeli mia mbili Katika vipimo vya sasa ni sawa na "kilo mbili na nusu" # Kwa kiwango cha kipimo cha mfalme Mfalme alikuwa na kipimo kilichoamua kiwango cha uzito wa shekeli, uzito mwingine na vipimo vingine. # Walizaliwa kwa Absalomu wana watatu na binti mmoja Inamaanisha Absalomu alikuwa na watoto watatu wa kiume na binti mmoja.