# Tafadhari usinifiche neno lolote nikuulizalo Muundo wa kinyume umetumika hapa ili kusisitiza na unaweza kuelelezwa kwa muundo chanya. Yaani "tafadhari niambie ukweli kuhusu lolote ninalokuuliza" # Je si mkono wa Yoabu uliopamoja nawe katika hili Hapa neno "mkono" linaonesha ushawishi wa Yoabu. # Kama uishivyo "Hakika kama uishivyo." Hapa mwanamke analinganisha uhakika wa alichokisema Daudi amesema kwa hakika kwamba anaishi, ili kusisitiza jinsi taarifa ilivyo ya kweli # Hakuna awezaye kuelekea mkono wa kulia... mfalme alivyosema Hapa mwanamke anaeleza ugumu wa kuongea na mfalme na kumficha asigundue ukweli kwa kulinganisha na mtu asivyoweza kuelekea upande wowote. # Mkono wa kulia au wa kushoto Taarifa inatoa milengo miwili na inamaanisha "popote." # Bwana wangu ni mwelevu Bwana wangu mfalme ni mwenye hekima" # Ni mwenye hekima, kama hekima ya malaika wa Mungu Mwanamke analinganisha hekima ya Daudi na ya malaika kusisitiza jinsi alivyo mwenye hekima.