# Basi Neno hili linatumika hapa kuonesha kikomo katika habari kuu. Hapa mwandishi anazungumzia mtu mwingine katika habari. # Seruya Hili ni jina la mwanamme # Kufahamu Hii inamaana kuwa Yoabu alitambua alichokuwa anafikiri Daudi. # akapeleka neno Tekoa na kutaka mwanamke mwerevu aletwe. Hii inamaanisha kuwa alituma mtu akiwa na ujumbe huko Tekoa na kumletea mwanamke. # Tekoa Hili ni jina la eneo # Uwe kama mwanamke aliyeomboleza Yoabu anatoa mlinganisho, akieleza kwa mwanamke jinsi alivyomtaka aonekane. # aliyekufa Hii inarejea kwa mtu aliyekufa, siyo wafu wote kwa jumla.