# Hivyo ikawa "Ikatukia." Kifungu hiki kimetumika kutambulisha tukio linalofuata katika habari. # Njiani "kusafiri njiani" # Habari ikamfikia Daudi kusema Hapa inasema kwamba habari ilikuja,mtu alikuja na kumwambia Daudi ile habari. # Ndipo mfalme alipoinuka "Kisha mfalme akainuka" # akachana nguo zake, na kulala juu ya sakafu Alifanya hivi kuonesha kwamba alikuwa na huzuni sana. # pamoja na nguo zao zimechanwa Walifanya hivi kuonesha huzuni yao na kuomboleza pamoja na mfalme.