# Daudi akatuma neno Hii inamaanisha kwamba alituma mjumbe kuongea na Tamari # Donge Mchanganyiko wa unga na maji unaotumika kwa kuokea. # Kuukanda Kutumia mikono kulichanganya donge # mbele yake Hii inamaanisha kwamba Tamari alitengeneza mkate mbele ya Amnoni. # Hivyo kila mtu akatoka "Kutoka nje kwa mtu" inamaanisha kuwaacha.