# Yoabu akapigana... akaukamata Hapa mwandishi anasema "Yoabu" lakini anarejerea kwa Yoabu na askari waliopigana pamoja naye. # Raba Kupigana dhidi ya mji hu, halisia inamaanisha kupigana dhidi ya watu wa Raba. # Hivyo Yoabu akatuma wajumbe kwa Daudi na kusema "Hivyo Yoabu akatuma wajumbe kwa Daudi kumwambia" # Wamechukua sehemu ya kusambaza maji mjini "Kukamata" eneo inamaanisha kuchukua umilki. # Kupiga kambi kinyume Hii inamaanisha kuzunguka na kushambulia. # Nimepigana... nimekamata... ikiwa nitachukua Hapa Yoabu anajisemea mwenyewe wakati halisia anarejerea kwake na askari wake. # Uchukue... chukua mji "Kuchukua" eneo inamaanisha kuchukua umilki. # Utaitwa Hii inaweza kuelezwa katika muundo tendaji. Yaani "watu watauita"