# Kusihi Kuombeleza au kuomba kwa hamu kubwa # kwenda ndani Daudi alikwenda ndani ya chumba chake alipokuwa peke yake. # Kumwinua kutoka sakafuni " na kumsihi kuinuka kutoka chini" # Ikawa "Ilitokea" # Hakuisikiliza sauti yetu Hapa "sauti" inasisitiza kwamba walikuwa wakiongea. # Siku ya saba Hii ni siku ya saba tangu mtoto azaliwe # Tazama Usemi unatumika kuwafanya watu wawe "makini" # Je atajitendeaje ikiwa tutamwambia kwmba mtoto amekufa?! Watumishi wanauliza swali hili kuonesha hofu yao. Yaani "tunaogopa kwamba anaweza kujidhuru ikiwa tutamwambia kwamba mtoto amekufa!"