# Hivyo kwa nini umedharau... Yahwe, hata kufanya maovu mbele zake? Swali hili linatumika kumkemea Daudi. Yaani "haukupaswa kumdharau ... Yahwe na kufanya yaliyomaovu mbele zake!" # Hata kufanya yaliyomaovu mbele zake "Mbele" ya Yahwe inarejea kwa kile anachofikiri. Hii inazungumzia anachohesabu kuwa uovu halisi. # Umemwua Uria Mhiti kwa upanga Daudi hakumwua Uria kwa mkono wake, bali alipanga Uria alivyouawa. Kifungu "kwa upanga" kinaonesha jinsi alivyokufa vitani. # Ulimwua kwa upanga wa jeshi la Amoni Inaonesha kwamba Daudi hakumwua kwa mkono wake bali alipanga jinsi ya kuuawa kwa Uria mkononi mwa Waamoni. # Upanga hautaondoka nyumbani mwako Hapa neno "upanga" linaonesha watu wanaokufa vitani. "Nyumba" ya Daudi inarejerea wazawa wake.