# Ni nani aliyemwua Abimeleki mwana wa Yerubeshethi? Yoabu anasema Daudi anaweza kumkemea kwa kuuliza swali hili. Yafaa kuwa "Kumbuka jinsi Abimeleki mwana wa Yerubeshethi alivyouawa!" # Abimeleki mwana wa Yerubeshethi Hili ni jina la mwanaume. Babaye anajulikana pia kwa jina la Gideoni. # Je mwanamke hakurusha jiwe la juu la kusagia juu yake kutoka ukutani hivyo kwamba alikufa katika Thebezi? Yoabu anasema Daudi aweza kumkemea kwa kuuliza swali. Yafaa kuwa "Kumbuka alikufa huko Thebezi mwanamke aliporusha jiwe la juu la kusagia juu yake kutokea ukutani" # kutokea ukutani "kutokea juu ya ukuta wa mji" # Jiwe la kusagia nafaka Jiwe zito ambalo lingeweza kuzunguka, lililotumika kwa kusaga nafaka ili kutengeneza mkate # Thebezi Hili ni jina la mji. # Kwa nini mliukaribia ukuta kiasi hicho? "Hamkupaswa kuwa mmeukaribia ukuta kiasi hicho!"