# Bwana wake Neno "yake" inarejerea kwa Uria na neno "bwana" inarejerea kwa Daudi. # Je haujatoka safarini? Kwa nini haukwenda nyumbani kwako? Hili swali linaonesha ushangao wa Uria kwa nini hakumtembelea mke wake. # Israeli na Yuda Hii inarejea kwa majeshi yao yaani "majeshi ya Israeli na Yuda" # Jinsi gani basi mimi naweza kwenda kwangu... pamoja na mke wangu? Swali hili linasisitiza hali ya Uria kukataa kumtembelea mke wake. # Kwa hakika kama uishivyo, sitafanya hivyo. Uria anaapa kwa ahadi yenye nguvu kwamba hatakwenda nyumbani kwa mke wake kwa vile askari wengine wapo vitani.