# Kisha Daudi akatuma Hapa neno "kutuma" inamaanisha kwamba Daudi alituma mjumbe. # Yoabu anaendeleaje, jeshi linaendeleaje, na vita inaendeleaje Daudi alikuwa akiuliza ikiwa Yoabu na jeshi walikuwa wanaendelea vema na kuhusu maendeleo ya vita. # Shuka nyumbani kwako Maana pendekezwa kwa kifungu "shuka chini" ni 1) Nyumba ya Uria ilikuwa chini kuliko kasiri la Daudi au 2) Nyumba ya Uria ilikuwa na umuhimu mdogo kulinganisha na kasiri la mfalme. # Nawa miguu yako Kifungu hiki kinamaanisha kurudi nyumbani kupumzika wakati wa usiku baada ya kufanya kazi mchana kutwa. # Mfalme alituma zawadi kwa Uria Daudi alituma mtu kupeleka zawadi kwa Uria.