# Maelezo ya Jumla Daudi aliendelea kuongea na Yahwe. # Hivyo basi Hapa "basi" haimaanishi "sasa," lakini inatumika kuleta usikivu kwa jambo muhimu kama ifuatavyo. # Na ahadi uliyoifanya kuhusu mtumishi wako na familia yake iwe imara daima Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. Yaani: "Na ufanye ulichoniahidi na familia yangu, na ahadi yako isibadilike" # mtumishi wako na familia yake Daudi anajisema katika nafsi ya tatu. Yaweza kuwa: "mimi na familia yangu" # Jina lako na liwe kuu daima Hapa "jina" inawakilisha heshima ya Yahwe. # Nyumba yangu, Daudi, mtumishi wako Hapa "nyumba" inawakilisha familia. # Umethibitishwa mbele yako Hii yaweza kuwa "ni salama kwa sababu wewe" au "unaendelea kwa sababu yako"