# Ikawa Kifungu kinaonesha mwanzo wa habari nyingine. # alipewa kupumzika kutokana na adui wote waliomzunguka "kupewa usalama kutokana na adui wote waliomzunguka." Hapa "pumziko" ni jina dhahania. Yaani: "kusababisha makundi ya maadui kuacha kushambulia Israeli" # Ninaishi katika nyumba ya mwerezi Mwerezi ni aina ya mti unaojulikana kwa uimara. Ni sawa na mninga katika utamaduni wetu. Inaaweza kuwa: "Ninaishi katika nyumba nzuri na ya kudumu" # sanduku la Mungu linakaa katikati ya hema Hema ni makazi ya muda. Yaani: sanduku la Mungu lakaa katika eneo la muda"