# tu nyama na mfupa wako Kifungu kinamaanisha "undugu." Yaani "sisi tunauhusiano nawe" au sisi tu wa familia moja." # wakati mfupi uliopita Hii ni habari ya kihistoria. Sauli alikuwa mfalme wao kabla ya Daudi. # Utawachunga watu wangu Israeli, nawe utakuwa mtawala juu ya Israeli Vishazi viwili hivi vinamaanisha kimsingi jambo moja na linasistiza kwamba Yahwe alikuwa amemchagua Daudi kuwa mfalme. # Utawachunga watu wngu Israeli Hapa kuwatawala watu kunazungumzwa kana kwamba ni kuwachunga. Yaani: "utawaangalia watu wangu Israeli" au "Utatawala juu ya Israeli watu wangu"